23 Novemba 2012 - 20:30

Viongozi wa Palestina baada ya ushindi dhidi ya Mazayuni walieleza kua himaya ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran ndio sababu ya ushindi na twashukuru kwa hilo.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Khalid Al-Batsh mmoja kati ya Viongozi wa Jihad Al-Islam alisema: Ujumbe wetu kwa Umma wa Kiislamu na Waarabu ni kwamba lazima tujifunze kuiga Iran kwa kuhami Wapalestina, himaya yao imezaa ushindi ulokuwa hautarajiwi.

Khalid Al-Batsh alitaka Waarabu na Umma wa Kiislamu kusaidia Palestina Silaha na fedha na kutaka Umma kufahamu rasmi Kundi la Jihad Al-Islam.

Talal Abu Dharifa alisema: Ushindi wa Palestina hasa Ghaza ni jambo muhimu kwa Wananchi wa Palestina, na ushindi huu ni ishara ya kuonyesha muungano wa makundi ya Kisiasa umefikia kileleni.

Khidr Habib Kiongozi wa Jihad Al-Islam nae pia alisema: Ushindi wa Ghazi ni wahistoria na lazima tusighafiliki kwa walosaidia katika ushidi huu Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran ilisaidia kwa hali na mali ili kuhakiki ushindi Ghaza, na tunaishukuru Iran kwa himaya yao, na himaya yao itaendelea hadi Palestina itolewe mikononi mwa Mazayuni.

Daud Shahab: Ushindi wa Ghaza ni ushindi wa Wananchi wapalestina, na bila shaka hatuwezi kufumbia macho himaya ya Iran katika ushindi huu, kwani Iran ilikuwa ni mwandalizi mkuu wa ushindi huu wa Kihistoria.

Aihab Al-Ghasib mzungumzaji wa Serikali ya Palestina Ghaza alisema: Leo sote tumeshuhudia ushindi wa Palestina dhidi ya adui yake Israel, na mlishuhudia vipi Wapalestina walishinda Walowezi kwa maana ya neno na leo hii imeshandikwa katika historia.